Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ushindi walioupata nchini Botswana ulitokana na maandalizi ya kisaikolojia aliyofanya kwa wachezaji wake kuelekea mchezo huo
Zahera amesema waliingia kwenye mchezo wakiwa na lengo la kufunga bao mapema kama ilivyokuwa kwa Rollers walivyokuja Dar
"Niliwaambia wachezaji kama wao walifunga kwetu na sisi ni lazima tufunge kwao," amesema
"Na baada ya kufunga niliwaambia ni lazima wote tujilinde kuhakikisha hawafungi"
"Ulikuwa ni mpango wetu kuwaacha wamiliki mpira na sisi tutumie mashambulizi ya kushitukiza"
Yanga imefuzu raundi ya kwanza ya michuano hiyo ikiwa imelipa kisasi kwa Rollers ambao waliwatoa mwaka jana
Yanga sasa itacheza na ZESCO United iliyoichapa Green Mamba mabao 3-0
No comments:
Post a Comment