Wakili Mwandamizi wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi,Erick Kabendera bado haujakamilika.
Simon ameeleza hayo leo Jumatatu Agosti 19, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mmbando
Mbali na upelelezi kutokamilika, Pia, hakimu anayesikiliza kesi hiyo, AugustineRwizile amepata udhuru.
Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi kiasi cha Tsh. Milioni 173,247,047.02, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu Makosa ambayo hayana dhamana
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 30, 2019 itakapotajwa tena.
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 30, 2019 itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment