We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, August 1, 2019

Kama alivyosema Makonda ''Wameoga'' - Kamwelwe

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amemuomba Rais Magufuli uwekwe utaratibu kwa ajili ya kulifanyia ukarabati wa Jengo la pili la Abiria ili liwe na uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi.

Waziri Kamwelwe ameyabainisha hayo leo Agosti 1 wakati wa uzinduzi wa Jengo la tatu la abiria (Terminal III) katika uwanja wa ndege wa julius Nyerere.
'Ombi langu kwako Mh Rais,  jengo lile Terminali II  linahitaji mambo mawili, moja  kuikarabati ipendeze kama ambavyo wamependeza wananchi waliokusanyika hapa kama alivyosema Makonda ''Wameoga'',lifanyiwe marekebisho ili nalenyewe ling'are  kama jengo la tatu lilivyo, pili katika kukarabati huko liongezewa capacity ikiwezekana mara mbili badala ya kubeba abiria milioni 1.5 libebe abiria milioni 3'' amesema Waziri Kamwelwe.
Jengo la tatu la abiria (TERMINAL III) katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 560 na litakuwa na uwezo wa kubeba abiria milioni 6 kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list