We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, August 21, 2019

Jerry Muro arejea Yanga 'kiaina'

Aliyewahi kuwa Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, amesema atajitolea kutoa hamasa kwa mashabiki ili kurudisha 'ari' ya miaka iliyopita
Muro alikuwa machachari wakati wa Uwenyekiti wa Yusufu Manji ambapo kwa kiasi kikubwa aliweza kufanya 'amsha-amsha' za nguvu na kuwafanya mashabiki wawe karibu na timu yao kila iliposhuka dimbani
Muro amejipambanua kumudu vyema kazi hiyo ya usemaji, juzi wakati Yanga ilipocheza na Polisi Tanzania mchezo wa kirafiki alipata wasaa wa kurejesha enzi zake;
"Yanga ni timu ya Wananchi, iliundwa na wafanyabishara wadogo wadogo, kiufupi wananchi wa kawaida"
"Hao Simba wanakosea kujiita timu ya Wananchi, yao ni timu ya ma Bwanyenye... Iliundwa na wageni, na ndio maana mwanzoni walijiita Sunderland"
"Hata mpaka leo wanaongozwa na ma Bwanyenye..(anawataja viongozi wa Simba) sababu asili ya timu yao ni ya ma Bwanyenye..!," ni miongoni mwa kauli zake ambazo zimezua tafrani kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya mashabiki wa Yanga wakilitumia neno 'bwanyenye' kuwatania wenzao wa Simba kuwa ni ma Bwanyenye Fc
Muro ndiye aliyeasisi majina mengi ya utani ambayo mashabiki wa Yanga hutumia kuwatania wenzao wa Simba

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list