Baada ya kushinda tenda ya kutengeneza na kusambaza jezi za Yanga, kampuni ya GMS imeendelea kumwaga fedha zaidi Jangwani baada ya kuingia mkataba wa matangazo ya magodoro ya GSM Foam yanayotengenezwa na kampuni hiyo
GSM kupitia magodoro yao ya GSM Foam, wameongeza idadi ya wadhamini kwenye klabu ya Yanga wakiungana na Sportpesa, Taifa Gas na Maji ya Afya
Kuongezeka kwa wadhamini ni habari njema kwa Yanga kwani udhamini huo unaingizia timu fedha na kujiweka kwenye mazingira mazuri kiuchumi
Kupitia wadhamini wake, Yanga ina uhakika wa kuingiza zaidi ya Bilioni moja kwa mwaka fedha ambazo zinatosha kulipa mishahara ya wachezaji
No comments:
Post a Comment