We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, August 1, 2019

BREAKING: BABA LEVO AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI MITANO

Mahakama ya Mwanzo ya Mwandiga mkoani Kigoma imeamuru kwenda jela miezi 5 Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini, Claiton Levocatus Chipando (Baba levo), kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama barabarani, Msafiri Ponera.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Frolence Ikorongo amesema Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kujiridhisha bila shaka, kwa kutumia ushahidi wa upande wa mlalamikaji, na kutupilia mbali utetezi wa Baba levo.
Awali Mahakama ilitoa uamuzi wa mshtakiwa Baba Levo, kwenda jela mwaka 1 ndipo akajitetea kwa kuiomba Mahakama impunguzie adhabu, kwani anategemewa na watoto 4 pamoja na  wananchi zaidi ya 25000.
Baba Levo ameendelea kujitetea kuwa endapo atafungwa mwaka 1 atapoteza sifa za kuendelea kuwa Diwani, hivyo ataisababishia Serikali hasara ya kufanya uchaguzi upya, na kwamba ni mara ya kwanza kukutwa na kosa la shambulio
 
Baada ya Hakimu kusikiliza utetezi huo akaamua kupunguza adhabu na kuamuru kwenda jela miezi 5, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list