Baada ya kufanya mazoezi ya peke yake kwa siku mbili, kiungo fundi wa mpira Ibrahim Ajib Migomba leo amejumuishwa kwenye mazoezi ya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo Jumapili
Ajib amejumuishwa kikosini baada ya madaktari kujiridhisha kuwa amepona kabisa majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na yuko tayari kuwakabili UD Songo
Hatma yake kuelekea mchezo wa Jumapili pamoja na mlinda lango Aishi Manula, iko mikononi mwa Aussems
No comments:
Post a Comment