Yanga huenda ikaumana na Rayon Sports August 04 kwenye mchezo wa kuhitimisha kilele cha wiki ya Mwananchi 'MWANANCHI DAY', imefahamika
Baada ya AS Vita kuondoa ushiriki wake kutokana na kubanwa na ratiba, Yanga imelazimika kutafuta timu mbadala itakayokuja kupamba tukio hilo
Rayon Sports imekiri kupokea mwaliko kutoka kwa klabu ya Yanga na huenda ikaja nchini kushiriki kwenye tukio hilo la kihistoria
Uongozi wa Yanga utazungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine, huenda ikaweka hadharani timu itakayokuja nchini August 04
No comments:
Post a Comment