We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, July 17, 2019

Yanga yafunga mjadala wa kocha Msaidizi

Uongozi wa Yanga umesema kocha Noel Mwandila ataendelea kuwa kocha Msaidizi wa timu hiyo akiwa ni pendekezo la kocha Mwinyi Zahera
Awali Yanga ilikuwa na mchakato wa kusaka kocha Msaidizi Mzawa ambaye angesaidiana na Zahera
Hata hivyo Zahera alipinga mchakato huo akitoa sababu zake
Kwanza alisema hapendi kuchaguliwa kocha Msaidizi, kuwa ni yeye aliyepaswa kupendekeza Msaidizi wake kama kulikuwa na ulazima wa kufanya hivyo
Lakini pia akasema wachezaji wa Kitanzania anawafahamu tabia zao, akiwa na kocha Msaidizi mzawa inaweza kuwa changamoto kwa kocha huyo
Mwisho alisema amefanya kazi na Mwandila kwa msimu mmoja, ameridhishwa na uwezo wake na angependa aendelee na majukumu hayo
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema wamekubaliana na kocha Zahera hivyo Mwandila ataendelea kuhudumu nafasi ya kocha Msaidizi
"Hakuna kitu kibaya ambacho kocha anachukia kama kupangiwa wasaidizi wake, wachezaji wa kuwasajili na kikosi," amesema Dk Msolla
"Kabla hajaondoka mimi nilikaa nae tukazungumza kuhusu benchi la ufundi, alichosema atabaki na msaidizi wake lakini kutakuwa na mabadiliko kidogo ambayo anayafanyia kazi sasa hivi"
cut
Mwandila alikuja nchini mwishoni mwa mwaka 2016 akiletwa na Kocha George Lwandamina akiwa kocha wa viungo
Hata hivyo baada ya kuondoka Lwandamina, Mwandila alikaimu nafasi ya kocha Mkuu mpaka pale alipokuja kocha Mwinyi Zahera
Kwa sasa Mwandila yuko mkoani Morogoro akikinoa kikosi cha Yanga wakati huu ambao Zahera yuko mapumziko nchini Ufaransa baada ya kumaliza majuku ya michuano ya Afcon 2019 na kikosi cha DR Congo
Hata hivyo Zahera anatarajiwa kurejea nchini kabla ya mwishoni mwa wiki

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list