Amesema wanachama hao wanapokumbushwa wajibu wao na kuachana na tabia hiyo wanageuka mbogo na kuanza kuzungumza mambo yasiyofaa kusaka huruma ya watu.
Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 23, 2019 mkoani Dodoma wakati akizungumza na wanachama wa CCM mkoani humo katika uzinduzi wa vibanda vya biashara.
Dk Bashiru amesema baada ya watu hao kubanwa na mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli wanazungumza ujinga nje ya utaratibu wa chama hicho.
Amesema miaka ya nyuma walikuwepo waliotafuna fedha na kuifanya akaunti ya CCM kwa mwaka kuwa na Sh5milioni, wakati hivi sasa kwa mwaka akaunti inakuwa na hadi Sh20 bilioni.
Amebainisha kuwa watu wa aina hiyo hawatavumiliwa, watashughulikiwa na kuwataka waondoke wenyewe kuliko kuendelea kukivuruga chama, “Chama hakiwezi kucheza ngoma ya kitoto.”
No comments:
Post a Comment