Simba leo imecheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki nchini Afrika Kusini baada ya kujifua kwa wiki moja
Imecheza na timu ya Chuo Kikuu cha Orbit Tvet katika mchezo ambao umepigwa kwa vipindi vitatu vya dakika 30
Nahodha John Bocco ambaye anatarajiwa kurejea nchini leo kujiunga na kambi ya timu ya Taifa pamoja na nyota wengine sita, ameifungia Simba mabao mawili kati ya manne iliyofunga
Simba ilifunga mabao yake matatu dakika za 9', 23' na 28'
Hassani Dilunga alifunga bao la pili wakati bao la nne lilifungwa na Wilker Da Silva kwenye dakika ya 64
No comments:
Post a Comment