We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 22, 2019

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATATU

Klabu ya ligi ya Uchina Beijing Guoan wamepania kumsajili winga wa Real Madrid Gareth Bale. Klabu hiyo, ina mpango wa kumfanya winga huyo mwenye miaka 30 kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya Uchina. (telegraph)
Manchester United, ambao awali walikuwa wakimnyemelea Bale wamejitoa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo. (Manchester Evening News).
Man United hatimaye imekubali masharti ya kumsajili beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atawasili katika uwanja wa Old Trafford kwa dau la £80m . (Bleacher Report)

Harry MaguireHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Kolscielny amekubali kujiunga na klabu ya Rennes. (RMC Sport).
Arsenal inatarajiwa kuishinda Tottenham katika kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos. Mchezaji huyo wa Uhispania atajiunga kwa mkopo.(Mirror)
Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza James Milner ,33, amesema hajui hatma yake katika klabu hiyo licha ya kwamba anataka kusalia. (Liverpool Echo)

James MilnerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Bayern Munich wanapigiwa upatu kumsaini winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha ,26, baada ya kushindwa kumsaini Leroy Sane na Gareth Bale. (90min)
Ombi la Crystal Palace la £20m kumsaini beki wa Uingereza Reece James limekataliwa na Chelsea. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alihudumu msimu uliopita akiichezea Wigan.(Star)
Arsenal, Chelsea, Manchester United na West Ham wote wana hamu ya kumsajili mchezaji wa Dynamo Kiev na Ukraine Mykola Shaparenko. (Caught Offside)

Wilfried Zaha

Real Madrid wamekataa ofa sita za kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, ambaye anahusishwa na uhamsho wa kuelekea Liverpool. (Cadena SAR)

TETESI ZA SOKA JUMAPILI


iwobi

Winga wa Nigeria na Arsenal Alex Iwobi ameonya kuihama Arsenal iwapo mchezaji anayedaiwa kuwa na thamani ya $80m Wilfried Zaha atajiunga na Arsenal na kuchukua nafasi yake
Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anafikiria kumsajili Andy Caroll kurudi katika klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 na raia wa Uingereza yuko huru baada ya kuachiwa na klabu ya West Ham mnamo mwezi Juni. (Sun on Sunday)
Mshambuliaji wa Tottenham na Uholanzi Vincent Janssen 25 anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa kuelekea katika timu ya Mexico Monterrey mapema wiki ijayo.(Football London)
Mlinda lango wa Uhispania David De Gea 28 amekubali kuandikisha kandarasi mpya ya miaka sita ambayo itamfanya kuwa mlinda lango anayelipwa mshahara mkubwa duniani.(Sunday Telegraph
Manchesater City inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa ArgentinaThiago Almada, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Velez Sarsfield nyumbani kwao. Mabingwa hao wa Premia wameripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa takriban £16m . (Sun on Sunday)

Kipa wa Man United David De Gea

Manchester United imeimarisha mazungumzo na Lille kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast Nicolas Pepe kwa dau la £70m. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amevutia hamu kutoka Liverpool , Arsenal na Everton.(Sunday Times)
Arsenal ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Itali Moise Kean, 19, na tayari wamewasiliana na ajenti wake (Mail on Sunday)
Watford wameanza mazungumzo na klabu ya Ufaransa Rennes kuhusu uwezekano wa kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 21 kutoka Senegal Ismaila Sarr. (Sky Sports)

Ismael SarrHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Newcastle ina hamu ya kumsajili winga wa Burnley anayedaiwa kuwa na thamani ya £30m Dwight McNeil, lakini mkufunzi mpya Steve Bruce amejiandaa kutoa ofa ya £15m. (Sun on Sunday)
Aston Villa inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kasimpasa na Misri Egypt Trezeguet, 24, katika makubaliano ya thamani ya £8.75m. (Sunday Telegraph)
Crystal Palace imefanya mazungumzo na Liverpool kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mchezaji mwenye umri wa miaka 28 Nathaniel Clyne. The Eagles wanataka raia huyo wa Uingereza ambaye aliichezea Bournemouth kwa mkopo msimu uliopita kuchukua nafais yake Aaron Wan-Bissaka, ambaye alijiunga na Manchester United mwezi June. (Mail on Sunday)
Beki wa Saint-Etienne na Ufaransa William Saliba, 18, atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya Jumanne katika klabu ya Arsenal kabla ya uhamisho wake wa £28m (Sunday Mirror)

Salliba

Tottenham italazimika kulipa £67m iwapo watamsajili kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Giovani lo Celso, 23, msimu huu . (Evening Standard)
Sheffield United na Aston Villa zote zina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford Neal Maupay. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ufaransa ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na timu hiyo. (Sun on Sunday)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried ZahaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha

Everton wako tayari kuipa changamoto Arsenal kumuwania mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, ambaye anauzwa na klabu yake ya Crystal Palace kwa kitita cha pauni milioni 80. (Evening Standard)
Manchester United, Everton na Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Juventus kuhusu kumsajili Blaise Matuidi. (Le Parisien)
Manchester United wanaongeza jitihadi kumpata kiungo wa Lazio, mzaliwa wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic. (Mirror)
Inter Milan wanamtaka mchezaji wa Man United Lukaku.
Livepool inamtaka beki wa kushoto wa Augsburg Philipp Max, 25, (Sport)

Mchezaji wa Real Sociedad Diego LlorenteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa Real Sociedad Diego Llorente

Tottenham na West Ham wanamtolea macho Diego Llorente, 25 wa Real Sociedad. (El Mundo Deportivo)
Wolverhampton Wanderers wanataka kumsajili mshambuliaji wa Italia na AC Milan Patrick Cutrone mwenye thamani ya takriban pauni milioni 20. (Express & Star)
Tottenham imempa mkataba mpya wa mwaka mmoja mshambuliaji Fernando Llorente. (Mail)
Crystal Palace imetangaza dau la pauni la milioni 8 kumpata kiungo wa Everton James McCarthy. (Sky Sports)
Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amemaliza matumaini ya Everton kwa kumsajili Kurt Zouma ambaye aliutumia msimu uliopita akiwa Goodison Park kwa mkopo. (Mirror)

Kocha wa Chelsea Frank Lampard
Image captionKocha wa Chelsea Frank Lampard

Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko, 33, huenda akaondoka Roma baada ya miaka mitatu, huku Inter Milan ikiwa na mpango wa kupata saini ya mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 15.(Sportitalia)
Mchezaji wa Chelsea, 18, Ethan Ampadu amefanya vipimo vya kiafya kabla ya kuhamia RB Leipzig ya Ujerumani. . (Sky Sports)
Klabu ya Brugge ya Ubelgiji ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Brighton na timu ya taifa ya Afrika Kusini Percy Tau, aliyecheza michuano ya kombe la mataifa Afrika. (Argus)
Derby County inataka kumsajili mlinda mlango wa Watford Daniel Bachmann, 25, kwa mkopo. (Derby Telegraph)

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list