We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, July 16, 2019

Simba yawatimua nyota 13, Okwi, Zana out


Simba imetangaza kuwaacha wachezaji wake 13, akiwemo mfungaji bora wa Uganda katika fainali za Afcon, Emmanuel Okwi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema kati ya wachezaji hao, sita wametolewa kwa mkopo na saba wamemaliza mikataba.
"Waliomaliza mikataba klabu haikuhitaji kuendelea nao, isipokuwa Asante Kwasi ambaye mkataba wake unamalizika Novemba.
"Kwasi amepata timu na klabu tumeamua kuachana naye baada ya makubaliano ya pande zote mbili ili akaendelee na maisha mengine," alisema Magori.
Aliwataja wachezaji wengine walioachwa rasmi kuwa Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Nicholaus Gyan, Zana Coulibaly, Nicolaus Kotei na Salim Mbonde.
Wachezaji waliowatoa kwa mkopo ni Mohamed Ibrahim (Mo), Marcel Kaheza, Mohamed Rashid, Adam Salamba, Paul Bukaba na Abdul Athumani wa timu ya vijana ya U20."Mbonde hatukutaka kumuacha, lakini mwalimu amependekeza kutokana na ushindani wa Simba ni bora aende kwenye timu nyingine ili akapate nafasi ya kucheza na kuendeleza kiwango chake," alisema Magori.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list