We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 22, 2019

Katibu mkuu wa CECAFA Musonye azipiga dongo lingine Simba na Yanga

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye amezijia juu kwa mara nyingine klabu za Simba na Yanga kufuatia kutohudhuria michuano ya Kagame Cup iliyomalizika hapo jana.

Akizungumza baada ya fainali ya Kagame Cup kati ya Azam FC na KCCA ya Uganda, Musonye ameendele kusisitiza kuwa kutokuwepo kwa klabu za Simba na Yanga hajaathiri chochote katika michuano hiyo, akisema kuwa klabu hizo ziachwe ziendelee kuzunguka nchi za wengine huku zikiacha mashindano kwenye ukanda wao.
"Nawaambia Simba na Yanga kwamba hata kama hawakuja watambue sisi hatukumuomba mtu, tuna timu nyingi sana za kujaza nafasi hizo. Wao waende huko Afrika Kusini, Uturuki wakaangalie majumba na takataka zingine zilizopo huko", amesema Musonye.
"Kwanza kuna pre-season gani nzuri ambayo walitakiwa kuwa nayo zaidi ya hii?, yaani unaogopa kushindana, unakwenda kucheza mechi za kirafiki ambazo hazina maana. Serikali ya Rwanda imeandaa kila kitu hapa imesema njooni mcheze, wewe hutaki unakwenda Afrika Kusini kutembea", ameongeza.
Michuano ya CECAFA Kagame Cup imemalizika rasmi jana kwa mchezo wa fainali kupigwa, ambapo KCCA ya Uganda imefanikiwa kunyakuwa ubingwa kwa kuifunga Azam FC bao 1-0. Katika mchezo wa mshindi wa tatu, Green Eagles imeshinda kwa 2-0 dhidi ya AS Maniema Union.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list