Rais Magufuli ameagiza Dkt. James Mataragio arejeshwe katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), baada ya kusimamishwa kazi tangu Agosti 2016.
Agizo hilo amelitoa leo Julai 22, 2019 kupitia taarifa ya Ikulu ambayo imeeleza kuwa Rais, ameitaka Wizara ya Nishati kumrejesha kazini Mkurugenzi huyo Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.
Dkt. James Mataragio alisimamishwa kazi Agosti 20, 2016, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, lakini Rais amesema arudishwe kazini aendelee na majukumu yake mara moja.
Chini ni Taarifa ya Ikulu.
No comments:
Post a Comment