Uongozi wa klabu ya Yanga umesema hauna pingamizi kwa kiungo wake chipukizi Maka Edward ambaye anaondoka kuelekea Lativia alikopata timu ambapo ametakiwa akafanyiwe vipimo vya afya
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema sera ya timu hiyo ni kuwapa fursa wachezaji vijana ili waonekane ili wapate nafasi ya kwenda kucheza soka nje ya nchi
Mwakalebela amesema Yanga imemruhusu Maka kwenda kujaribu bahati yake huko Lativia na anaamini mafanikio yake yatakuwa manufaaa kwa Yanga na timu ya Taifa
Maka aliyekuwa bado na mkataba na Yanga, amewaomba wapenzi, mashabiki na Wanachama wa Yanga wamuombee ili aweze kufanikiwa
No comments:
Post a Comment