Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mkataba wa nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib unamalizika mwishoni mwa mwezi huu na mazungumzo ya kuhuisha mkataba wake yalifanyika
Akijibu maswali ya waandishi Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam leo, Mwakalebela amesema Yanga ilifanya mazungumzo na kiungo huyo lakini wamemuachia mwenyewe aamue hatma yake
"Mkataba wake unamalizika mwisho wa mwezi huu, mazungumzo yamefanyika na klabu imempa nafasi ya kuamua kama anapenda kubaki nafasi ipo,lakini kama anataka kuondoka klabu inamtakia kila la kheri"
"Tunatambua Ajib ni mchezaji mzuri na tungependa kuendelea nae lakini uamuzi wa kubaki au kuondoka upo mikononi mwake"

No comments:
Post a Comment