Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu wakati mchakato wa usajili ukiendelea
Mpaka sasa Simba haijaweka hadharani 'vifaa' vyake vipya pamoja na taarifa kuhusu usajili kwa ujumla
Hali hiyo imepelekea wasiwasi miongoni mwa mashabiki wa Simba ambao wamezoea mabingwa hao wa Tanzania Bara kutamba kwenye dirisha la usajili
Hata hivyo Mo amesema michakato ya usajili tayari imeanza na siku si nyingi wataweka hadharani wachezaji ambao wamesajiliwa
"Kwa sasa tunaendelea na usajili, tumebadilisha utaratibu wetu wa jinsi ya kuendesha mambo yetu lakini siku sio nyingi kila kitu kitawekwa hadharani," amesema Mo
Baada ya kujitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame, Simba inatarajiwa kuingia kambini mapema ambapo inaelezwa kocha Patrick Aussems atalazimika kukatisha likizo yake kuwahi kambi
Kuanza mapema kwa michuano ya ligi ya mabingwa kunatajwa kuwa sababu ya mabingwa hao wa nchi kuamua kuingia kambini mapema
Simba inaweza kuweka kambi Ureno au Marekani ingawa benchi la ufundi ndilo litakalotoa mapendekezo ya mwisho
No comments:
Post a Comment