Bunge limeelezwa hayo leo Ijumaa Juni 21, 2019 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Olenasha kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalum (CUF), Rukia Kassim Ahmed.
Katika swali la msingi Rukia amesema mazingira ya kufanya biashara nchini ni magumu na kutaka kujua ni lini Serikali itaondoa urasimu ili wananchi waweze kunufaika.
Katika majibu yake, Ole nasha amesema mbali na tozo hizo, mapendekezo ya kuondolewa tozo nyingine kupita muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2019 yamewasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango.
“Moja kati ya mafanikio ya jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara ni kwa Tanzania kuendelea kuongoza kwa uwezo wa kuvuta mitaji kutoka nje katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki tangu mwaka 2012.”
“Kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji ya dunia inayotolewa na shirika la biashara na maendeleo la umoja wa mataifa ya mwaka 2018. Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa kuvutia mitaji ya jumla ya Dola 1,180 za Marekani ikifuatiwa na Uganda,” amesema Olenasha.

No comments:
Post a Comment