WAKATI Yanga ikiendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji na tayari ikiwa na mazungumzo na makipa wawili Singida imepeleka maombi ya kutaka kipa Klaus Kindoki achukuliwe kwa mkopo.
Kumekuwa taarifa kuwa huenda Yanga ikaachana na kipa huyo kutokana na kutofanya vizuri kwa msimu ambao umemalizika ambapo alitumika baada ya Beno Kakolanya kutimka.
Taarifa za ndani zinadai kuwa Singida iko kwenye mpango wa kufanya mazungumzo na Yanga kama watamuacha Kindoki basi wao wamchukue hata kwa mkopo. Festo Sanga Mkurugenzi wa Singida alisema :” Usajili sisi bado mambo yakiwa tayari tutaweka wazi.”
No comments:
Post a Comment