Wito huo umekuja muda mfupi baada ya Rungwe akiwa miongoni mwa wawakilishi wa vyama vya upinzani vinane kumaliza mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Chaumma Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi wengine walikuwa wakitoka kwenye vyama vya Vyama vya ACT Wazalendo, CCK, Chadema, DP, NCCR Mageuzi, NLD na UPDP.
Katika mkutano huo, viongozi wa vyama hivyo walitoa tamko la kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio utakaofanyika katika kata 32 Juni 15, 2019, kwa madai unasimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na Manispaa kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu.
Alipoulizwa kwa simu, Rungwe alikiri kupokea wito huo wa Polisi.
“Ni kweli nimepewa wito natakiwa kuripoti kituo cha Polisi Oysterbay kesho saa 4 asubuhi,” amesema
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mussa Taibu hakutaka kuwa wazi juu ya wito huo huku akimtaka mwandishi kumfuatilia kiongozi huyo atakapokwenda kituoni hapo kesho.
“Kwani kama ameitwa kuna tatizo gani? uje ufuatilie atakapokuwa ameitwa,” amesema RPC Taibu.
Taarifa iliyotolewa na mjumbe wa Sekretarieti ya Ushirikiano wa Vyama hivyo, Eugene Kabendera leo Juni 2, imesema askari wa Polisi wakiwa kwenye magari matatu, walifika Ofisi ya Chaumma iliyopo Kijitonyama Dar es Salaam na kumpa taarifa Rungwe.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment