Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amekamatwa na polisi akiwa hotelini jijini Paris.
Kwa mujibu wa jarida la Jeune Afrique, Ahmad alikamatwa saa 8:30 am katika hotel Berri jijini Paris, na polisi wa kupambana na makosa ya matumizi mabaya ya fedha na rushwa (Oclif).
Wamesema kukamatwa kwake kunatokana na madai ya matumizi mabaya na rushwa katika kampuni ya Ufaransa ya Tactical Steel.
Katibu mkuu wa zamani wa CAF, Amr Fahmy alimshutumu Ahmad kwa kutoa rushwa kabla ya kutimuliwa kwake Aprili.
Katika taarifa ya Fahmy aliyoituma kwa kitengo cha uchunguzi FIFA alimshutumu rais huyo kuongeza gharama ya ziada ya dola 830,000 katika vifaa alivyoagiza kwa Tactical Steel.
Rais wa Tactical Steel, Sabine Seillier alisisitiza kuwa kampuni yake ilifanya kila kitu kwa uwazi katika kushinda tenda hiyo. Alisema kampuni yake iliyoa garati ya kukabidhi vifaa hivyo ndani ya muda wa wiki tatu.
Kukamatwa huko kwa Ahmad kumekuja siku moja baada ya shirikisho hilo kutoa uamuzi tata wa kurudiwa kwa mchezo wa pili wa hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Esperance ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco baada ya mchezo wa kwanza kuvunjika.Wakati alipoulizwa kama Tactical Steel inausika katika mpango wa kuwahonga Ahmad au shirikisho lake, Seillier alijibu: “Siyo kweli. Tactical Steel inafuata sharia za Ufaransa.”
Mechi hiyo ilivunjika kutokana na Wydad kugomea kuendelea na mchezo mara baada ya kukataliwa kwa bao lao lililofungwa dakika ya 58 na Walid El Karti huku pia mwamuzi Bakary Gassama kutoka Gambia akigoma kutazama marudio kwenye teknolojia ya usaidizi ya video na hata pale alipoamua kufanya hivyo, mfumo ulidaiwa kuharibika.
No comments:
Post a Comment