We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, June 10, 2019

Maalim Seif, wenzake wapewa majukumu ACT-Wazalendo



Miezi mitatu baada aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake kujiondoa kwenye chama hicho na kutimkia chama cha ACT-Wazalendo, sasa wamepewa majukumu ndani ya chama hicho.

Maalim Seif na wenzake walijitoa CUF Machi 2019 baada ya kushindwa kesi waliyofungua Mahakama Kuu wakipinga uongozi wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na mgogoro ulioanza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Juni 10, 2019 na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, Ado Shaibu, kufuatia kikao cha kamati kuu ya ACT Wazalendo kilichoketi Dar es Salaam jana Jumapili, imesema Maalim Seif mwenye kadi namba moja ya chama hicho, ameteuliwa kuwa mshauri mkuu wa chama.
Katika nafasi za kamati kuu ya chama hicho, wafuasi wa Maalim Seif wameingizwa akiwemo Fatma Fereji na Eddy Riyami, huku pia kukiwa na wajumbe wengine waliongezwa ambao ni Theopista Kumwenda na Mwajabu Dhahabu.
Katika nafasi za wenyeviti wa Kamati za Kitaifa, Nassor Marzurui ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi, huku Salim Bimani akiteuliwa kuwa  Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Mawasiliano na Uenezi na Joram Bashange akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya kampeni na uchaguzi.
Wengine ni pamoja na Ismail Jussa aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mikakati, usimamizi na ufuatiliaji, huku mbunge wa zamani wa viti maalum. Mhonga Ruhwanya akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya oganaizesheni, mafunzo na wanachama.
Kwa upande wa makatibu wa kamati za kitaifa, Shaweji Mketo aliyekuwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF, ameteuliwa kuwa Katibu wa kamati ya oganaizesheni, mafunzo na wanachama wa chama hicho, huku Kulthum Mchuchuli akiteuliwa kuwa katibu wa kamati ya Katiba na Sheria.
Wengine ni pamoja na Mbarala Maharagande aliyeuliwa kuwa katibu wa kamati ya uadilifu na Rachel Kimambo akiteuliwa kuwa katibu wa kamati ya mikakati, usimamizi na ufuatiliaji.
Chama hicho kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kilipata umaarufu baada ya Maalim Seif na wenzake kuhamia wakitokea CUF.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list