We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

Kigwangalla ampa ofa Diatta wa Senegal

Mchezaji wa Senegal Krepin Diatta, ambaye alifunga goli la pili la Senegal kwenye mchezo wa kwanza wa AFCON dhidi ya Tanzania, amekaribishwa kuja kutalii nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Waziri Kigwangalla amemkaribisha mchezaji huyo, Krepin Diatta, kuja Tanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na serikali itagharamia gharama.
"Nitumie nafasi hii kukukaribisha Krepin Diatta kuja Tanzania kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo imetoka kutuzwa kuwa bora zaidi barani Afrika na Pori la Akiba kubwa zaidi Afrika, Selous. Tutagharamia safari yako hiyo," aliandika Kigwangalla kupitia Instagram.
Diatta alitawala katika mitandao ya kijamii hapa nchini baada ya kuifungia Senegal goli la pili katika mechi hiyo wiki iliyopita. "Waafrika wote ni ndugu na hata hii mipaka tunayoiona iliwekwa na wakoloni waliotutawala'', aliongeza Waziri.
"Nitumie nafasi hii kukukaribisha Krepin Diatta kuja Tanzania kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo imetoka kutuzwa kuwa bora zaidi barani Afrika na Pori la Akiba kubwa zaidi Afrika, Selous. Tutagharamia safari yako hiyo," aliandika Kigwangalla.
Diatta anachezea klabu ya Brugge ya Ubelgiji anakocheza nahodha wa Taifa Stars,  Mbwana Samatta, alieleza kusikitishwa na picha zake kusambaa mitandaoni kwa lengo la kumdharirisha.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list