We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 21, 2019

Hakuna haja ya kuwa na ukomo wa wachezaji wa kigeni - Nkamia

Mbunge wa Jimbo la Nchemba Juma Nkamia wakati akichangia bajeti kuu ya serikali ameishauri serikali kuangalia namna ya kutoza kodi kwa wahezaji wanaotoka nje ya Tanzania wanaokuja kucheza vilabu vya hapa nyumbani.
Nkamia aamesema serikali ikiweka utaratibu huo pia itaweza kuondoa zuio la kila timu kuwa na ukomo wa idadi ya wachezaji kutoka nje kwa sababu wachezaji hao watakuwa na faida kwa nchi.
"Ipo haja kwa Tanzania kuangalia nchi hii itafaidika namna gani na wachezaji wanaocheza mpira wa kulipwa. Sioni sababu ya kuzuia kuwa na wachezaji 10 au zaidi wa kigeni lakini bado tunaweza kupata mapato makubwa kutokana na wachezaji hawa."
"Leo hii mchezaji anasajiliwa Tanzania kwa milioni 80 lakini halipi kodi, analipwa mshahara wa dola za Marekani 15,000 kwa mwezi lakini halipi kodi. Ipo haja sasa kwa serikali kuangalia namna gani itapata kodi za wachezaji."
"Naamini serikali ikiweka mfumo mzuri wa kupanga kodi kwa wachezaji hata hii hoja ya kwamba tuwe na wachezaji watano itaondoka."
"Kwa mfano England kombe la dunia lililopita ilifika nusu fainali lakini haijaweka ukomo wa wachezaji wa kigeni kwa hiyo tufikirie hatuna sababu ya kuweka ukomo wa idadi ya wachezaji wa kigeni Tanzania sio kisiwa."
"Hata UEFA Champions League na Europa League timu zote za England zimefika fainali lakini hawana ukomo wa wachezaji wa kigeni."
"Tuweke utaratibu wa kupata kodi za wachezaji hawa badala ya kuwazuia wasije.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list