Na Ahmad Mmow, Lindi.
Baada ya baadhi ya wanachama wake kujiunga na chama cha ACT-Wazelendo, leo wanachama wengine wanatarajiwa kujiunga rasmi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).
Taarifa za kuaminika toka ndani ya CHADEMA zimeeleza kwamba wanachama wa CUF wanatarajiwa kukabidhiwa kadi na mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Leo katika ofisi ya CHADEMA wilaya ya Lindi. '' Jana mheshimiwa Barwany alijiunga nasi wakati wa kikao, leo atawaongoza wenzake takribani 60 kukabidhiwa rasmi kadi.
Nimatunda ya operesheni ya CHADEMA ni msingi inayoendelea katika mkoa huu wa Lindi,'' Muungwana Blog ilidokezwa na mmoja wa viongozi ambao hakutaka jina lake liandikwe. Jana wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na mwenyekiti Mbowe ilitaarifiwa aliyekuwa mbunge wa Lindi (2010-2015), Salum Barwany alijiunga na CHADEMA.
No comments:
Post a Comment