Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) limewataarifu vijana wote wa chama hicho kuwa tayari muda wowote kutekeleza maagizo ya viongozi wao huku wakililalamikia Jeshi la Polisi kwa kutomwachia kiongozi wa baraza hilo, Patrick Ole Sosopi pamoja na Daniel Naftal.
BAVICHA imesema kuwa imesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kumkamata Mwenyekiti wa baraza hilo pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Kwela mwaka 2015 kupitia CHADEMA, Daniel Naftal Ngogo.
Viongozi hao walikamatwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Ifakara na baadaye kuhamishiwa katika kituo cha polisi kati mkoani Morogoro kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuanza shughuli za kampeni za kisiasa kabla ya muda.
Kupitia barua iliyosainiwa na Katibu Mwenezi wa BAVICHA, Edward Simbeye imemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa kumwachia kiongozi wao kwani hakuna kosa alilotenda kwa mujibu wa sheria.
Isome barua yao hapa chini.
No comments:
Post a Comment