Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike amewaengua wachezaji saba katika kikosi chake kinachoelekea Misri leo kuendelea na maandalizi ya michuano ya AFCON 2019
Wachezaji walioachwa kwenye kikosi cha wachezaji 32 wanaoelekea Misri ni Jonas Mkude, Ibrahimu Ajibu, Ayoub Lyanga, Ally Khamis, Kenned Wilson na Shomari Kapombe.
Amunike amesema kwamba kigezo kilichotumika kuwaacha nyota hao ni kiwango chao mazoezini na nidhamu.
Stars inasafiri na jumla ya wachezaji 32 kwenda Misri kabla ya kuchujwa katika hatua ya mwisho na kubaki 23
No comments:
Post a Comment