Kiungo mpya wa Yanga Issa Birigimana amepinga madai ya klabu ya APR kuwa bado ana mkataba na timu hiyo mpaka mwaka 2020
Juzi viongozi wa timu hiyo walidai kuwa yungali na mkataba wa mwaka mmoja hivyo kuitaka Yanga kufuata taratibu za kumsajili
Hata hivyo Birigimana amepinga madai hayo akisisitiza mkataba wake ulikuwa umemalizika kilichokuwepo ni mazungumzo ya kuongeza mkataba zoezi ambalo halikufanyika kwa kuwa aliamua kujiunga na Yanga
"Unajua huku Rwanda mashabiki wamechukia kuona naondoka, APR walitaka kunipa mkataba mrefu na nikawaambia wasubiri kwanza nimalizane na mechi iliyobaki," Birigimana amenukuliwa na Mwanaspoti
"Niliamua kutulia kwanza ili kuona mazungumzo na Yanga yataishia wapi, lakini tumemaliza vyema na nimesaini mkataba wa kufanya kazi;
"Mabosi wa Yanga waliniuliza mapema kuhusiana na mkataba wangu na nakala ninazo hapa. Viongozi wa APR wamepatwa hasira, hivyo Yanga wasihofu mimi ni mchezaji wao"
Birigimana amesisitiza kuwa hata Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) linafahamu kuhusiana na mkataba wake kwa kuwa kuna nakala halisi.
Jana Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alisema timu hiyo ilikuwa tayari kufanya mazungumzo na APR ili kutatua mgogoro huo (kama upo)
No comments:
Post a Comment