Zahera : Nimetembea Afrika sijaona timu inawashabiki kama Yanga
Jana klabu ya Yanga ilitumia kufanya uzinduzi wa kampeni yao ya kuichangia Yanga katika jiji la Dodoma mchongo mzima ukifanyika katika hoteli ya Morena.
Moja ya wahudhuriaji wa uzinduzi huo alikuwepo kocha mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi ambapo katika uzinduzi huo alifunguka kuwa amezunguka Afrika lakini hajaona timu yenye washabiki wengi kama Yanga.
“Katika muda niliofanya kazi hapa, nimesoma na kujifunza vitu vingi sana. . hata kwa hiki nnachoshuhudia leo hakika kimenipa hamasa sana! msimu ujao hatutoumia. .
Nimetembea karibu nchi zote za Afrika nikiwa na timu ya Taifa, nawahakikishieni hakuna hata nchi moja yenye mashabiki kama hawa wa Yanga, hata TP Mazembe haina fanbase kubwa kama Yanga.
Nimetembea karibu nchi zote za Afrika nikiwa na timu ya Taifa, nawahakikishieni hakuna hata nchi moja yenye mashabiki kama hawa wa Yanga, hata TP Mazembe haina fanbase kubwa kama Yanga.
Najiuliza kuna ulazima gani timu kama hii eti kungoja tajiri mmoja aje awekeze pesa zake?wakati wenyewe mnasema hii ni timu ya wananchi? kwanini wananchi tusiibebe timu yetu wenyewe? sasa tunapaswa kuibeba wenyewe. . timu kama Yanga SC inapaswa kushindania makombe makubwa Afrika. .Naomba tuichangie Yanga” -Mwinyi Zahera.
No comments:
Post a Comment