Beki kisiki wa Simba Serge Paschal Wawa jana alilazimika kutoka kwenye dakika ya sita mchezo dhidi ya TP Mazembe baada ya kupata maumuvu ya mguu
Wawa amesema maumivu hayo yalimfanya ashindwe kuendelea na mchezo hata hivyo aliwapongeza wachezaji wenzie kwa kufanikiwa kumaliza mchezo huo bila ya kuruhusu bao
Wawa amesema atarejea kikosini hivi karibuni lakini huenda akaukosa mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki ijayo Lubumbashi, DRC
"Nilitoka uwanjani na kuiacha timu yangu inapambana, walinihitaji lakini sikuweza kuendelea kutokana na maumivu niliyokuwanayo hata wakati natembea nilikuwa napata maumivu makali," alisema Wawa
"Ingawa ninamaumivu makali namwachia Mungu, naamini nitarejea uwanjani hivi karibuni.
"Mchezo wa marudiano utakuwa mgumu lakini ninaimani na wachezaji wenzangu na timu nzima kwa ujumla"
Baada ya Wawa kutoka, nafasi yake ilichukuliwa na Juuko Murshid ambaye alicheza vyema sambamba na kiraka Erasto Nyoni

No comments:
Post a Comment