Mshambuliaji Kinda wa Tanzania, Yohana Nkomola amefanikiwa kujiunga na klabu ya Arsenal Kiev inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ukraine kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kufanikiwa majaribio katika timu hiyo.

Akizungumza na www.eatv.tv, kaka wa mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, Stanley Nkomola amesema kuwa mchezaji huyo alikwenda kwenye majaribio katika klabu hiyo pamoja na beki wa Mtibwa Sugar, Nikson Kibabage Lakini Mkomola akapata bahati ya Kufuzu majaribio hayo.
Yohana Nkomola ni miongoni kwa wachezaji waliwahi kuichezea Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, katika mashindano ya AFCON nchini Gabon mwaka 2017 na baadaye alisajiwa na Yanga Sc.
Kwa pindi chote ambacho alicheza Yanga, Nkomola hakupata nafasi ya kutosha ya kucheza, ambapo baadaye aliamua kuvunja mkataba na mabingwa hao wa kihistoria nchini.
No comments:
Post a Comment