We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, April 5, 2019

Kuna tatizo la watu kubambikiziwa kesi na kufungwa bila hatia - Dk. Mahiga



Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Augustine Mahiga amesema kuwa tatizo la watu kubambikiziwa kesi na kufungwa bila hatia, kunatokana na kutojua sheria na haki zao za msingi.

Amesema ili kumaliza tatizo hilo, jitihada zaidi zinahitajika kwa watoa huduma za msaada wa kisheria kusaidia kutoa elimu kwa jamii.

Dk. Mahiga aliyasema hayo Jijini Arusha wakati alipohudhuria kongamano la watoa huduma za msaada wa kisheria Tanzania lililohudhuriwa na mashirika 88 ya watoa huduma kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Aliyataka mashirika yanayotoa msaada wa kisheria nchini kufichua vitendo vya watu kubambikiwa kesi na kufungwa bila hatia kwani vinaliaibisha Taifa na kupunguza nguvu kazi inayotegemewa na jamii. "Wapo watu waliofungwa kimakosa kwa kutojua haki zao za kisheria hivyo mashirika na Taasisi yanayojihusisha kutoa huduma za kisheria lazima yaongeze jitihada zaidi ili kufichua masuala ya ubambikizaji wa kesi,"alisema Waziri.

Aliongeza kuwa serikali inawatambua na kuwathamini watoa huduma za msaada wa kisheria Tanzania na imeandaa mpango utakaowasaidia katika utekelezaji wa majukumu yako kwani kazi wanayoifanya wamekuwa wakijitolea zaidi.

Awali, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome aliyataka mashirika yanayojihusisha na huduma za msaada wa kisheria kutotumia fani hiyo kuendesha harakati za kisiasa.

Alisema huduma wanayoitoa ilenge kuwasaidia wananchi kupunguza migogoro hasa ya ardhi ambayo imekithiri katika maeneo ya mikoa mingi nchini. Naye, Msajili wa Huduma za Msaada wa Kisheria, Felister Joseph kutoka Wizara ya Sheria na Katiba alisema hadi sasa kuna jumla ya wasajili wasaidizi wapatao 4,500 nchini na lengo ni kuanzisha mfumo wa mashirikiano kwenye maeneo yao ya kazi kati ya watoa huduma wasaidizi wanasheria na taasisi za serikali.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list