Na Ferdinand Shayo,Arusha
Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Hamphrey Polepole amewapokea madiwani watatu wa Wilaya Karatu wakitokea Chadema ambapo wamekabidhiwa kadi na kujiunga rasmi katika Chama cha Mapinduzi.
Aidha polepole amesema kuwa chama hicho hakitawapokea wanachama ambao hawana sifa ya uadilifu na uwajibikaji na wamekua wakijihusisha na vitendo vichafu ili kuhakikisha kuwa chama hicho kinalinda hadhi yake.
Pia ameagiza kusimamishwa kwa bodi ya maji ya KAVIWASU ambayo imekua ikiwauzia wananchi maji kwa bei ya juu .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare amewataka WanaCcm kuungana n kuhakikisha kuwa chama hicho kinashinda uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020.
Kwa upande wao madiwani waliojiunga na CCM wamesema kuwa kasi ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo imewavutia kuungana na wanachama wenzake kuleta maendeleo.
Madiwani wa tatu wa Chadema wamepokelewa CCM akiwemo Diwani Daa Benedikto Modaha ,Diwani wa Ganako Lazaro Simon Bajuta,Diwani wa MbuluMbulu Amani Joseph .
No comments:
Post a Comment