Kupitia mahojiano aliyofanya Miss Tanzania 2000 Jacquline Mengi leo April 5,2019 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM amefunguka ishu ya kupenda urembo kuhusika na suala zima la muonekano wa ndevu za mume wake Dr. Reginald Mengi.
Jacquline Mengi ameongeza na kusisitiza kuwa watu wasipende kumuhukumu mtu kwa jinsi anavyonekana na kuweka wazi ni takribani miaka tisa sasa tokea awe kwenye mahusiano ya kimapenzi na mume wake na kumalizia kwa kusema pesa sio kila kwenye mapenzi.
Fahamu vitu vitano alivyovizungumza Jacquline Mengi kwenye kipindi cha XXL
“Usimuhukumu mtu kwa mtu unavyomuona, mume wangu ukimuona na ukimjua ni tofauti, Mimi na Mume wangu tumekuwa kwenye mahusiano karibia miaka 9 na ili muanze mahusiano ya kweli lazima muanze kama marafiki”
“Nilikutana na mume wangu wakati naenda London, ilikuwa kwenye ndege na tulizungumza maongezi ya kawaida na kuanzia hapo ndiyo tukaanza mawasiliano, kabla ya hapo sikuwahi kumuona popote”
“Mimi napenda urembo na ni sehemu ya maisha yangu, kila ninachofanya huwa tunafanya wote na hiyo nimemuambukiza hata yeye kwani ninachokipenda na anachokipenda nakipenda na yeye anapenda, zile ni ndevu zake natural na hakuna dawa pale”
“Pesa sio kila kitu kwenye mahusiano maana Pesa inaweza kuwepo na kesho isiwepo naamini kikubwa ni unapokuwa kwenye mahusiano tafuta mtu ambaye ni rafiki kwako na mimi nasema kila siku Mume wangu ni rafiki yangu”
“Muda wa kuacha muziki ulikuwa umefika nilipata kitu kingine kwangu niliona ninakipenda zaidi na sikukosea, nilipoamua kusomea ‘Interior Design’ na kuanzisha kampuni nilifanya kitu roho inapenda kuimba ilikuwa ni ‘dream’ yangu ya utotoni namshukuru Mungu nilipata nafasi ya kutimiza ndoto yangu”
No comments:
Post a Comment