We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, April 6, 2019

Gadiel awashusha presha Yanga

BEKI wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael, aliyeukosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Ndanda FC juzi kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara, amerejea kuongezea nguvu kikosi chake.

Beki huyo alikosekana katika mchezo huo baada ya kuondoka wiki mbili zilizopita kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio ya soka la kulipwa katika timu ya Bidvest.
Lakini sasa beki huyo amerejea na anatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho kilichoshindwa kutamba dhidi ya Ndanda na sasa ataungana na wenzake mjini Mwanza, ambako kwa sasa ndio kuna uwanja wa nyumbani wa Yanga.

Baada ya sare hiyo, sasa Yanga watahamishia hasira zao kwa African Lyon, ambao watacheza nao Jumatatu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, badala ya Jumapili, siku ambayo Mbao FC wataikaribisha Azam FC kwenye uwanja huo.
Akizungumza naSI jana, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema nyota wao, Ibrahim Ajib, ataendelea kubaki Dar es Salaam kwa sababu bado hajapona jeraha lake la nyonga, lakini Gadiel, Haji Mwinyi, mlinda mlango Ramadhani Kabwili, Juma Abdul na Mohammed Issa ‘Mo Banka’ waliokosekana kwenye mechi zilizopita wataungana na timu.

Hafidh alisema pamoja na Ajib, nyota wengine watakaokosekana kwenye safari hiyo ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, anayetumikia adhabu ya mechi tatu, Baruani Akilimali, Maka Edward na Juma Mahadhi.
“Tunaondoka leo asubuhi na wachezaji 22 watakwenda na nyota sita watabaki Dar es Salaam kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo majeraha na wengine wana adhabu,” alisema Hafidh.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list