Baada ya Simba SC kutoka sare na TP Mazembe, Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kupata nyumbani sare sio nzuri ila ni hatua kubwa.
Manara amesema kuwa hakuna wakumlaumu zaidi ya wao kukosa bahati huku akiwaambia Wana -Simba kuwa game ya Lubumbashi ni ya Jasho na Damu.
"Kupata sare ya goalless nyumbani sio nzuri ila yana advantage kubwa kuliko tungepata sare ya magoli," ameandika Manara.
"Na leo niwaambie hakuna wa kumlaumu zaid ya cc kukosa bahati!! Niwaambie Wanasimba Game ya Lubumbashi ni ya Jasho na Damu!! Na Soka bado ipo wazi kwetu."
No comments:
Post a Comment