Baada ya kuunga mkono kauli ya RC Mkaonda kuwa Media zinawapa muda mwingi watu wanaofanya mambo ya kipuuzi na kuwafanya wawe maarufu badala ya kufanya hivyo kwa watu wanaofanya mambo ya msingi, hatimaye Shilole ameamua kumuomba radhi mlevi maarufu Tanzania Konki Liquid juu ya kauli yake ya jana usiku.
Shilole kwenye maelezo yake ya msamaha amesema kuwa ‘hakusoma mazingira’ na alijikuta akimbeza Pierre Liquid bila ya kujua anamuumiza kihisia.
KWA WATANZANIA WENZANGU,. KWANZA, NIKIRI KWAMBA NIMEONA WENGI NILIOWAKWAZA KUTOKANA NA MANENO NILIYOONGEA JANA KWENYE TUKIO LILIONDALIWA NA RAFIKI YETU @JOKATEMWEGELO(#TOKOMEZAZIROKISARAWE). KWA KUWAKWAZA HUKO BILA HATA KWENDA MBALI KUTOA MAELEZO YOYOTE, NAOMBA RADHI, MNISAMEHE SANA.PILI, NAHISI KUNA NAMNA SIJAELEWEKA AU MIMI SIKUWEKA VIZURI MAELEZO YANGU. NINYI MNANIJUA VIZURI, MWENZENU MIMI MARA NYINGI SANA NIMEONGEA VITU HADHARANI KWA KUKOSEA KUTOKANA NA UDHAIFU NA UWEZO WANGU MDOGO KWENYE KUJIELEZEA (HILO MNALIJUA, KWAMBA MIE MWENZENU KIDOGO SHULE SIKWENDA NA WAKATI MWINGINE KICHWA CHANGU KINAPATA MOTO NA HIYO SIO SIFA). SASA NAOMBA MNIRUHUSU KUELEZA KWA UFUPI NIA YANGU. HOJA YANGU MIMI ILIKUWA “KUNA VITU VYA MSINGI HAMZUNGUMZI ILA VITU VYA AJABU MNAZUNGUMZA…..” UKISIKILIZA ILE VIDEO UTASIKIA MSTARI HUO. HICHO NDIO KITU NLICHOTAKA KUELEZA, SIO KUMKASHIFU PIERRE AU MTU MWINGINE YEYOTE. IWAPO PIERRE NI MMOJA KATI YA WATU WALIOKWAZIKA, NAMUOMBA SANA ANISAMEHE. LAKINI TUWE WA KWELI, WATU WENGI WAMEWAHI KUSEMA HILI (KUNA VITU VYA MSINGI HAVITANGAZWI), ILA TU MIMI KWA AKILI YANGU NDOGO NILISHINDWA KUSOMA MAZINGIRA NA MUDA NIKALISEMA JANA. NIRUDIE TENA KUSEMA SAMAHANI.
NIMEONA WENGI WAKIRUDI NYUMA KUTAFUTA MATUKIO YANGU, KUTAFUTA NILITOKEA WAPI HADI HAPA NILIPO. NIWAHAKIKISHIE KWAMBA MIMI NAFAHAMU UPENDO MKUBWA WA WATANZANIA KWANGU KIASI KWAMBA WALINIBEBA HATA PALE NILIPOKOSEA, WALINIVUMILIA KATIKA UJINGA WANGU NA BADO WANAENDELEA KUNIVUMILIA, WANANIPENDA LICHA YA ULEWA WANGU MDOGO (KINGEREZA NA MAMBO MENGINE AMBAYO YAMEGEUKA UTANI DHIDI YANGU), NA WALINIPA NAFASI KUJIFUNZA, KUJIREKEBISHA NA KUKUA HADI HAPA NILIPO.NARUDIA TENA, NIMEKOSEA KAMA NILIVYOWAHI KUKOSEA MARA NYINGI, NAOMBA RADHI TENA, LAKINI ZAIDI YA YOTE NAOMBA MFAHAMU SIKUWA NA NIA MBAYA, NILIKOSEA TU NAMNA YA KUSEMA NA NISEME WAKATI GANI.
Tazama video hiyo ya Shilole akimnanga Pierre Liquid, kwenye hafla ya jana ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero.
No comments:
Post a Comment