Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewatahadharisha watu wote wanaomuunga mkono mnywaji wa pombe maarufu Tanzania, Konki Liquid kwa kuwambia kuwa waendelee kumsapoti lakini matokeo yake watayaona baadae.
RC Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika “Nawapongeza wote mnaunga mkono matendo ya watu kama hawa na kuyapa nafasi katika jamii. Najua kuelewa jambo inahitaji Muda .Ipo siku mtaelewa“.
Jana kwenye hafla ya harambee ya Tokomeza Zero ya DC Jokate, RC Makonda alivitaka vyombo vya habari viache kuwapa watu wenye sifa za ajabu kama akina Dkt. Shika na Konki Liquid na badala yake wawape airtime watu wanaofanya mambo makubwa kwenye jamii.
Kwa upande mwingine rapper Nikki wa Pili kutoka WEUSI yeye amempongeza Pierre Liquid kwa kumuita mnyaji anayejitambua kwani analewa na anafanya mambo ya muhimu kwenye jamii ikiwemo kuchangia elimu.
“Somo la piere kwa wanywaji woteee. …..usinywe ukaenda nyumbani ukampiga mkeo. …..kunywa lakini changia maendeleo ya elimu, amasisha elimu, amasisha michezo na uzalendo kwa timu yako. ……..lakini pia tizama fursa katika unywaji kama huwezi kua konki liquidii basi jadili michongo biashara na madili ukiwa katika unywaji. Ukiwa mnywaji wa namna hii utabaki juu ila ukinywa ukaharibu familia, ukachepuka, ukaharibu kazi, ukala mtaji wewe utabaki chiniiiii haulambi hata Lolo, Chiiiii konki fire,“ameandika Nikki wa Pili.
Jana Pierre Konki ni mmoja ya watu walijitokeza kwenye hafla ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero, ambayo pia ilihudhuriwa na RC Makonda.
No comments:
Post a Comment