Familia ya Ruge Mutahaba wamesema wanatambua Ruge aliwahi kuwakosea watu kwa kuwa yeye ni binadamu hajakamalika.
Mtoto mkubwa wa Ruge aitwaye Mwachi amesema Familia inaomba msamaha kwa niaba yake na imewasamehe wote waliomkosea pia.
“Ninamuombea msamaha baba yangu kwa wale wote aliowakosea enzi za uhai wake, nasi tunawasamehe wote waliomkosea baba,” amesema Mwachi wakati akisoma wasifu wa baba yake
Amesema baba yake alikuwa mtu aliyejitoa kwa wengine mpaka familia ilifikia wakati inaona watu wa nje wanamfaidi kuliko wao.
“Alitenga muda mwingi kusaidia kwa kuzingatia misingi ya utu, alipambana kwa hali zote kufanikisha mambo mengi katika jamii,” alisema huku akijitahidi kujizuia kutoa machozi.

No comments:
Post a Comment