Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa wiki moja kwa mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya umeme,kampuni ya State Grid Electrical and Technical Works kumaliza kazi ya kuunganisha umeme katika vijiji vya Mtama baada ya kuchelewa kumaliza kazi hiyo kwa takribani miezi sita.
Mgalu alitoa agizo hilo baada ya baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mihogoni kumlalamikia kuhusu kuchelewa kuunganishwa umeme katika vijiji vyao.
Wananchi hao walisema kuchelewa kwa mradi wa umeme katika eneo lao kunasababiswa na uzembe wa mkandarasi anayejenga mradi huo.
Walisema ni vyema serikali ikaangalia uwezekano wa kubadilisha makandarasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati
Baada ya kusikia malalamiko na maombi ya wananchi hao, Mgalu alisema serikali haiwezi kuwavumilia watendaji au wakandarasi wanaofanya kazi kwa mazoea. Kwahiyo mkandarasi huyo akamilishe zoezi la kupanda nguzo za umeme na kuwasha ndani ya siku saba alizompa.
Alisema serikali inatambua umeme ni biashara sio anasa,hivyo vijiji 30 vilivyopo kwenye mpango katika wilaya Lindi na 133 vya mkoa wote wa Lindi vitapate umeme.
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa kampuni ya State Grid Electrical and Technical Works Mhandisi, Bahati Manyangali alikiri kuwepo kwa ucheleweshaji wa umalizaji wa kazi hiyo.Hata hivyo alisena uchelewaji huo ulikotokana na sababu za kiufundi na kuchelewa nguzo za umeme
Alisema tayari kazi ya kupanda nguzo 10 kati ya 30 zinazotakiwa kupandwa katika kijiji cha Mihogoni imeanza.
No comments:
Post a Comment