Uongozi wa klabu ya Yanga, unalaani vikali kitendo cha kuchana jezi ya Simba kilichofanywa na baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa mashabiki wa Yanga.
Kitendo hicho kinachoonekana kwenye video, kikifanywa na watu waliovalia jezi za Yanga kinajenga taswira mbaya ya uhasama na chuki wakati Simba na Yanga ni watani wa Jadi wasiokuwa na uhasama wala chuki.
Kwa taarifa hii, Yanga inawataka mwanachama, mashabiki na wapenzi wake kote nchini na Duniani kutambua kwamba soka ni Mchezo wa uungwana, na kwamba hakuna tija yoyote kufanya vitendo vinavyoashiria kujenga uadui na chuki baina ya mashabiki wa soka.
"Kitendo hicho si cha kiungwana na si chakiuana michezo, hivyo uongozi wa Yanga unakilaani na kukemea vikali mashabiki na wapenzi wake kuihusisha na masuala kama hayo,"
Fredrick Mwakalebela.
Makamu Mwenyekiti- Yanga.
Makamu Mwenyekiti- Yanga.
No comments:
Post a Comment