Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo saa kumi jioni watashuka kwenye uwanja wa Taifa wa Botswana kuumana na Township Rollers katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa hatua ya awali
Yanga haihitaji matokeo mengine tofauti na ushindi au sare ya mabao zaidi ya moja ili iweze kutinga raundi ya kwanza
Ni mchezo usiotabirika, lakini kwa maandalizi yaliyofanywa na kikosi cha kocha Mwinyi Zahera, matumaini ya kuibuka na ushindi ni makubwa
Ugumu wa mchezo huo unakuja kutokana na kila timu kuhitaji matokeo
Township Rollers wana faida ya bao la ugenini lakini bao hilo bado haliwapi tiketi ya kufuzu mbele ya Yanga
Muhimu kwa vijana wa Zahera kupata bao la mapema ambalo linaweza kuwaondoa wapinzani wao mchezoni
Azam Tv watakuwa mbashara kupitia chaneli ya Azam Sport 2
Kila la kheri timu ya Wananchi..
No comments:
Post a Comment