Takribani wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi zinazodaiwa kuwa nafasi ya msemaji wa klabu ya Yanga inayoshikiliwa na Dismas Ten inakwenda kukabidhiwa kwa mtu mwingine.
Dismas Ten ameangushiwa jumba bovu kwa madai kuwa viatu vya usemaji wa klabu hiyo vinampwaya kutokana na kushindwa kwake kufanya hamasa ya watu kujitokeze kwa wingi katika michezo mbalimbali ya timu hiyo ukiwemo wa hivi karibuni dhidi Towship Rollers ya Botswana Klabu Bingwa Afrika uliopigwa uliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa taarifa za ndani inadaiwa kuwa Yanga SC inatarajia kumtangaza msemaji wake mpya ambaye ni Hassan Bumbuli atakayeweza kuchukua nafasi ya Dismas Ten.
Hasssan Bumbuli ni nani ?
Hassan Bumbuli ni mwanachma wa klabu ya Yanga, ambaye pia amekuwa katika kamati ya uhamasishaji wa timu hiyo katika tukio la hivi karibuni la tamasha la ‘Kubwa Kuliko’. Kitaaluma ni Mwandishi wa Habari lakini kwa sasa akiwa ni Mkurugenzi wa uwendeshaji wa Kampuni inayoitwa Rospa Media.
Mbali na kuwa Afisa habari ndani ya klabu ya Yanga, Dismas Ten inadaiwa kushika nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu kwa miamba hiyo ya soka Jangwani.
Taarifa za Hassan Bumbuli kuwa ndiye anaetarajiwa kuwa msemaji ndani ya Yanga zinazidi kushikahatamu baada ya hivi karibuni anaedaiwa naye kuwa msemaji mpya wa Klabu ya Simba ambaye anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni baada ya kupita kwa michezo ya Kimataifa, Gift Macha kuposti habari hii katika akaunti yake ya Instagram inayomtabiria mema mtani wake, Bumbuli.
”Unamfahamu huyu jamaa mwenye Tshirt ya Blue? Anaitwa Hassan Bumbuli.. Atakuwa mtu mkubwa pale Yanga hivi karibuni… Huyu mwenye jezi ya Taifa Stars ni mimi.. Nina Sapraizi kubwa kwenu.. Hivi karibuni.. Familia ya Kurasa za mwisho,” – Ameandika Gift Macha.
Gift Macha anakwenda kuchukua nafasi ya Haji Manara ndani ya klabu ya Simba, wakati Hassan Bumbuli anatua Jangwani kuchukua nafasi ya Dismas Ten Yanga SC.
Klabu za Simba SC na Yanga SC ni watani wajadi na wenye historia kubwa katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla na mara kadhaa mambo yao mengi hufanana, hivyo kama haya yanayodaiwa yatatimia katika siku hizi chache zijazo huwezi kushangaa kwa hasimu hawa kufanya mabadiliko kwa pamoja katika safu zao za Afisa habari.
No comments:
Post a Comment