Azam FC imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fasil Kenema FC ya Ethiopia katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ushindi huo unaipeleka Azam FC moja kwa moja kwenye hatua inayofuata kwa jumla ya magoli 3-2 kufutia kipigo cha bao 1-0 ilichokipata kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita nchini Ethiopia.
Magoli ya Azam kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Richard Djodi dakika ya 23 na 31 pamoja na Obrey Chirwa dakika ya 59 huku bao pekee la Kenema likifungwa na Mujib Kassim dakika ya 37.
Wakati Kenema wakifungashiwa virago, Azam wanasubiri kucheza na Triangle United ya Zimbabwe
Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya
No comments:
Post a Comment