Manchester United itakabiliwa na deni la mshahara la pauni milioni 12 kwa mchezaji Alexis Sanchez hata kama atasajiliwa na klabu ya Inter Milan. (ESPN)
Sanchez, 30, ambaye ni raia wa Colombia alikosa mazoezi ya Alhamisi na klabu yake ya Man United baada ya kwenda ubalozi wa Marekani jijini London. (Sun)
Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 28, na mlinzi raia wa England James Tomkins, 30, wapo katika mazungumzo ya kuongeza mikataba yao na klabu ya Crystal Palace. (Guardian)
Barcelona wamekataa ofa ya klabu ya Inter Milan ambao wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal, 32, kwa mkopo. (Mundo Deportivo)
Man United wapo ukingoni kukubali mapatano ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Tottenham na Uhispania Fernando Llorente, 34. (Gazzetta dello Sport - via Star)
Lille wanaamini kuwa watafanikiwa kumng'oa kiungo Mreno Renato Sanches, 22, kutoka Bayern Munich. (L'Equipe)
Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer ataweza kutumia kitita cha pauni milioni 75 kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari. Fedha hizo United walizipata baada ya kumuuza mshambuliaji raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, katika klabu ya Inter Milan mwanzoni mwa mwezi huu. (Talksport)
Kiungo Mreno wa klabu ya Leicester City Adrien Silva, 30, amesafiri kuelekea Monaco kwa ajili ya vipimo vya kiafya vitakavyofanyika leo Ijumaa. Silva anatarajiwa kujiunga na Monaco kwa mkopo. (Daily Telegraph)
Kipa wa Chelsea Muargentina Willy Caballero, 37, anatakiwa na klabu Real Madrid. (Marca - in Spanish)
Ujumbe wa wawakilishi wa Real Madrid upo Ufaransa kufanya majadiliano juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27 kutoka klabu ya Paris St-Germain. (Marca - in Spanish)
Winga raia wa Brazil anayekipiga na klabu ya Chelsea Kenedy, 23, anaangalia uwezekano wa kuihama moja kwa moja klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili la ulaya kufungwa wiki ijayo. (Goal)
Miamba ya Uturuki klabu ya Fenerbahce imejitenga na harakati za uhamisho wa beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 29. (Star)
No comments:
Post a Comment