Yanga haitaweza kumtumia mlinda lango wake namba moja Farouq Shikalo kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers baada ya Shirikisho la soka barani Afrika kushindwa kumpatia leseni
Hati ya uhamisho wa nyota huyo kutoka Bandari Fc ilichelewa kuifikia Yanga hivyo hakuandikishwa kwenye usajili wa CAF kwa wakati
Changamoto hiyo pia imewakuta beki Mustapha Suleyman na David Molinga ambao usajili wao umefanywa kwenye awamu ya tatu ya usajili wa CAF
Msimu huu CAF iliweka madirisha matatu ya usajili, dirisha la kwanza lilifungwa Julai 10 ambapo timu zilisajili bila faini
Dirisha la pili likafungwa Julai 21 ambapo timu zilipaswa kusajili kwa kulipa faini ya dola 250 kwa kila mchezaji atakayeandikishwa
Dirisha la tatu lilifungwa Julai 31 ambapo timu zilipaswa kulipa faini ya dola 500 kwa kila mchezaji aliyeandikishwa
Hata hivyo wachezaji wote walioandikishwa kwenye dirisha la tatu hawaruhusiwi kucheza raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kuwa Shikalo, Molinga na Mustapha hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo dhidi ya Township Rollers
Hata hivyo wachezaji hao wataruhusiwa kuitumikia Yanga kuanzia raundi inayofuata kama timu itafuzu
No comments:
Post a Comment