Msanii wa HipHop na mfanyabiashara Mwana Fa amefunguka suala zima la kulipiza kisasi, kwa mtu aliyemkosea na ishu za uwezo na bahati katika maisha.
Mwana Fa amezungumza hayo leo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kusema kulipiza kisasi ni imani ya mtu,
"Huwa nawapanga watu kwenye makundi nikigundua tunaishi vizuri nakuweka juu kama hatuwezani nakufungia vioo. Siwezi ku-deal na mtu asiye na maarifa, pia kila visasi vyangu ni kwa watu walionikosea kama nipo katika nafasi nita-deal nao tu, ila wakati mwingine wanasema kisasi ni chakula kizuri kukiacha kwa muda, baadae nakuja kukukata kichwa".
Aidha msanii huyo amezungumzia suala la kuweza na bahati katika maisha, ambapo amesema huwa anaamini katika kuweza kwa sababu ni kitu cha kudumu na mtu anatakiwa akifanye kwa uwezo, ufundi na ujuzi.
Pia ameendela kusema bahati ni muhimu sana katika maisha kwa sababu anaamini kuna watu wanaweza sana ila hawana bahati hivyo hupata wakati mgumu kwenye maisha yao.
No comments:
Post a Comment