Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara alipanga kuzungumza na wanahabari kuhusu hatma yake ndani ya Simba kufuatia ujio wa Gift Macha ambaye anatajwa kuchukua nafasi yake
Hata hivyo inaelezwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amemtaka Manara aendelee kufanya kazi Simba
Manara amefuta mpango wake wa kujitoa kunako klabu ya Simba
Ujumbe wa Manara:
"Boss wangu amezuia press yangu ya kesho na huyu ni mtu namheshimu sana"
"Niwahakikishie ntaendelea kufanya kazi katika Club hii ninayoishabikia sana"
"Sote sisi interest yetu ni Simba,hakuna kurudi nyuma hadi Wanasimba tutimize malengo yetu"
"Vita yetu sasa tuhamishie kwa Wabangu bangu.. Na tutawaambia kwa sauti kubwa
No comments:
Post a Comment