Mkutano wa 39 wa SADC uliokuwa ukiendelea jijini Dar es salaam umehitimishwa leo baada ya kufanyika kwa siku 2, ambapo kupitia Mwenyekiti wake Rais Dkt John Pombe Magufuli, amesema Jumuiya itaendelea kushirikiana kwa pamoja.
Akizungumza wakati akihitimisha mkutano huo Rais Magufuli ameeleza masuala mbalimbali ambayo Jumuiya hiyo wamekubaliana kwa pamoja ili kuleta maendeleo.
"Nitoe wito kwa Sekretaieti waendelee kutumia vizuri fedha zinazotolewa na wanachama wetu na washirika wa maendeleo, hivyo basi niwaombe matumizi hayo yapelekwe kwenye miradi ya maendeleo na yasiishie kwenye semina."amesema Rais Magufuli
"Napenda kuwaomba Viongozi tushirikiane kwa kuleta maendeleo, na niwaahidi Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Jumuiya tutashirikiana na wanachama katika kuleta maendeleo." amesema Rais Magufuli
No comments:
Post a Comment